Powered By Blogger

Thursday, March 22, 2012

JIHADHARI NA PROPAGANDA


WEDNESDAY, MARCH 21, 2012

MAJIMAREFU AWAKA KUUNGANISHWA NA NASSARI WA CHADEMA KATIKA PICHA ANAYODAI NI FEKI

'Picha hii nilipigwa nikiwa na huyu mbunge mwenzangu, Vicent Nyerere (kulia), lakini huyu wa kushoto (Joshua Nassari) hakuwepo karibu yangu kabisa! Yeye alikuwa mbali akiamrisha vijana wanichome moto tena akiwa na hasira, tofauti na anavyocheka katika picha hii. Huu ni mchezo mchafu wa kuunganisha picha kwenye kompyuta uliofanywa na CHADEMA na kwa makusudi gazeti hili likaichapisha, baada ya kuona kwamba hatua aliyofanya Nassari ya kutaka niuawe jana ni mbaya sana. Nitalishitaki gazeti hili". Analalamika Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani wakati akionyesha picha inayomuonyesha akiwa katika furaha ya hali ya juu yeye, Nyerere na Nassari. Picha hiyo imechapishwa leo ukurasa wa kwanza gazeti la Mwananchi.
Picha yenyewe anayolalamikia Profesa Majimarefu ndiyo hii kama tulivyojaribu kuinakili kutoka gazeti la mwananchi. Mdau hebu itazame kwa makini, je ni halisi au feki,  hasa ukitazama vizuri kwenye kwapa la Nassari lililokutana na Ngonyani? Pia tunamkaribisha mpigapicha wa picha hii, Edwin Mjwahuzi kama hatajali atupe picha 'orijino' ya hii tuliyonakili kwa ajili ya kuthibitisha ukweli.

Nukuu iliyojaa hekima
"Mtu mzima mwenye akili timamu akakushauri upuuzi ilhali anafahamu wazi kuwa wewe pia unazo akili timamu ukiukubali upuuzi wake atakudharau"

VIJEMBE KIKWELIKWELI


"Wenzetu alama yao ni kama kijiti hiki mnavyokiona!, achaneni nacho kitupeni, mpigieni kura Sioi alete maendeleo Arumeru." akasema Elirehema Kaaya ambaye naye 'alikula sahani moja' na Sioikwenye kura za maoni za CCM. Kushoto ni mratibu wa kampeni za CCM kitaifa Mwigulu

Nchemba akijibu tuhuma za chadema

Akizungumzia kuhusu CHADEMA kulalamikia Tume ya Uchaguzi kuwa haitawatendea haki kwenye uchaguzi huo, Mwigulu alisema, hata safu yao ya uonozi tangu Mwekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe hadi wabunge ikishika nafasi zote kwenye Tume hiyo CCM lazima itashinda uchaguzi wa Arumeru Mashariki utakaofanyika Aprili Mosi mwaka huu.
"Kwa Uchaguzi huu wa Arumeru Mashariki, hata Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilborod Slaa awe Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mbowe (Mweyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe) awe Mkurugenzi wa Uchaguzi, Zitto (Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Kabwe Zitto) awe Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi  na wabunge wote  wa CHADEMA  wawe wasimamizi wa uchaguzi huo, halafu CCM tuweke mawakala tu, naapa kikwetu CCM itashinda", alisema Mwigulu.

Alisema malalamiko ya CHADEMA dhidi ya vyombo vitakavyosimamia uchaguzi huo ni woga wa kushindwa kwa sababu wanafahamu kuwa CCM imejiimarisha vya kutosha Arumeru Mashariki na italirejesha jimbo.